Baada ya kushuhudia timu yetu ya Taifa, Taifa Stars, ikishindwa kufuzu kuingia katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, wengi wetu tutakuwa bado tunajiuliza swali lile lile kila wakati, NINI TATIZO?
Mwaka huu umekuwa wa ajabu baada ya miamba mingi ya Afrika nayo kushindwa kufuzu katika fainali hizo, ikiwemo Nigeria, Cameroon, Afrika Kusini na Misri. Lakini pamoja na jirani zetu wa Kenya na Uganda pia kushindwa kutimiza ndoto hizo, tuangalie hapa kwetu ni kipi hasa kinatufanya tunashindwa kufanya vizuri katika mashindano makubwa.
Tatizo ni makocha wanaoinoa timu yetu? Au ni wachezaji wenyewe? Au ni mfumo mzima wa mpira wetu hapa Tanzania?
Kwa pamoja, tuelekee chini ya muembe wa uwani tuongee kinaga ubaga, NINI TATIZO????…. Kandanda Forum
